Nafasi Ya Matangazo

July 29, 2015



 Na Mwandishi Wetu
Mchekeshaji maarufu Eric Omondi na bendi ya muziki ya SARABI kutoka Kenya wataungana na wanamuziki wa Tanzania Grace Matata na Leo Mkanyia na bendi yake ya Swahilli Blues kukonga nyonyo za mashabiki wa muziki na vichekesho jijini Dar es Salaam wakati wa onyesho la muziki jumamosi wiki hii.

Onyesho hilo ambalo limeandaliwa na CDEA:“Culture and Development East Africa” kwa kushirikiana na Nafasi Art Space litafanyika jumamosi ya tarehe moja mwezi wa nane mwaka huu, kuanzia saa moja jioni mpaka asubuhi katika ukumbi wa Nafasi Art Space-Mikocheni.

Mratibu wa onyesho hilo Naamala Samson alisema kuwa mbali na onyesho hilo pia kutakuwa na burudani kemkem kutoka kwa maDJ wa Santuri Safari kutoka Kenya na Uganda ambapo kiingilio kitakuwa ni shilingi 10,000/- kupata burudani za muziki wa bendi na kwa wale watakaoingia kwenye disco la kukesha ni shilingi 20,000/-, na tiketi za V.I.P zitauzwa kwa shilingi 40,000/-.

“Wanamuziki wote wamefanya mazoezi ya kutosha na wamejiandaa kikamilifu kwa onyesho hili la kihistoria, ni siku hiyo watanzania watapata fursa ya kuonja ladha ya muziki wa Afrika Mashariki wenye vionjo vya nyumbani na kupata vichekesho vya mwaka kutoka kwa Omondi” alisema Naamala.
Bendi ya Sarabi ni miongoni mwa bendi kubwa na zinazofanya vizuri nchini Kenya na kuwepo kwake kwenye tamasha hili kutanogesha mambo na kutoa burudani ya kutosha kwa wakazi wa Dar es Salaam na maeneo ya jirani.
Posted by MROKI On Wednesday, July 29, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo