Nafasi Ya Matangazo

January 02, 2013

Kwa taarifa zilizopatikana na za uhakika kutoka kwenye vyanzo vyetu vya habari,vinaeleza kuwa yule msanii aliyekuwa akisumbuliwa na matatizo ya kiafya kwa muda mrefu,Sadick Juma Kilowoko ama aliyetambulika sana katika tasnia ya Filamu hapa nchini kwa jina la kisanii Sajuki,ambaye hivi karibuni Serikali ilijitolea kubeba jukumu la kugharamia matibabu yake na hatimaye hivi karibuni kulazwa kwenye kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU) kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili,amefariki Dunia mapema leo asubuhi.

Mungu aipumzishe roho ya marehemu mahali pema peponi-Ameni.

Wadau tutazidi kutaarifiana kwa habari nyingine kuhusiana na msiba huu kwa kadiri zitakavyokuwa zikipatikana.
Posted by MROKI On Wednesday, January 02, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo