Nafasi Ya Matangazo

June 13, 2017

WATOTO watatu ambao  walipelekwa Marekani kwa ajili ya matibabu zaidi mara baada ya  kujeruhiwa katika ajali iliyotokea  hivi  huko karatu na kuhusisha vifo 32 vya wanafunzi pamoja na walimu  hali zao zinaendelea vizuri.

Majeruhi wawili kati yao wakiwa wamesharuhusiwa kutoka hospitalini na kupelekwa kituo maalum cha uangalizi ambacho wauguzi na madaktari watakuwa wanawaangalia kwa saa 24 na baada ya hapo watatoa maamuzi ya  kuwaruhusu kwenda nyumbani.

Aidha mtoto mmoja ambae ni Doreen  aliefanyiwa upasuajia maeneo mbali mbali kwenye mwili wake  amebaki katika wodi ya watoto katika  hospitali  ya Mercy kwa ajili ya kuendelea na matibabu ya karibu zaidi ambapo baada ya madaktari kuridhika na afya yake  nae watamruhusu.

Hayo yalisemwa  jana na Mbunge wa Singida Kaskazini,  Lazaro Nyalandu  ambae ni mmoja wa aliyefanikisha safari ya majeruhi hao,alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa kuhusiana na jinsi ambavyo hali za watoto hao zinaendelea.

Alisema watoto wawili walioruhusiwa ni  Sadia na Wilson ndio walioruhusiwa  kutoka hosptali na kupelekwa kwenye kituo maalum cha uangalizi.

Alisema kuwa mtoto doreen amebaki  kwenye wodi kutokana na  yeye kufanyiwa operesheni katika maeneo mengi ya mwili huku operesheni yake ikiwa imechukua muda wa saa saba tofauti na wenzake na kwamba mara baada ya madaktari kuridhika na uimara wake wa mfumo wa uti wa mgongo  ataruhusiwa kutoka kwenye hatua ya kwanza na kwenda hatua ya pili ambapo hadi sasa hali yake nae  inaendelea vizuri.

Nyalandu alidai kuwa yeye kama mtanzania aliyeguswa na ajali hiyo anazidi kuwashukuru sana watanzania wote kwa kuungana kwa pamoja kuwaombea watoto hao kwani Mungu amewaponya na anaamini watarejea tena ili kuweza  kuendelea  na masomo yao .

"Nichukue nafasi hii kuwashukuru sana watanzania waliowaombea watoto  hawa kwani matumaini makubwa yameonekana sana kwani naamini hatua waliyotoka hawa watoto ni kubwa sana na naamini baada ya kutoka hatua hii ya pili ya kuwa kwenye kituo maalum cha uangalizi wataruhiswa kwenda majumbani"aliongeza Nyalandu.

Aidha aliishukuru serikali kwa jitiada zote iliyofanya ya kuungana kwa pamoja kuwasafirisha watoto hao hadi Marekani ikiwa ni pamoja na kuwashukuru waliotoa ndege za kuwasafirisha pamoja na madaktari na wauguzi  wa hopitali ya mount meru ambao wamejitolea kuhudumia watoto.

Posted by MROKI On Tuesday, June 13, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo