Nafasi Ya Matangazo

March 22, 2017



Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika Kata ya Uyole mkoani Mbeya. Makalla amewataka watendaji wa serikali katika ngazi mbalimbali kuzishughulikia na kuzipatia majibu kero za wananchi kwa haraka.
Wananchi Kata ya Uyole wakiuliza maswali kuhusiana na kero zao mbalimbali kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya akimsikiliza Kamanda wa Polisi akijibu baadhi ya kero za wananchi.
MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amewataka watendaji wa serikali katika ngazi mbalimbali kuzishughulikia na kuzipatia majibu kero za wananchi kwa haraka.

Makalla aliyasema hayo wakati wa mkutano wake wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi Kata ya Uyole na kusema kufanya hivyo kutawafanya wananchi wazidi kuwa na imani nao na serikali kwa ujumla.

Mkutano huo wa hadhara ni muendelezo wa mikutano yake mbalimbali ya kusikiliza kero za wananchi na kuzioatia ufumbuzi jambo ambalo linasaidia kuondoa malalamiko ya wananchi.

“Watendaji wa serikali tunapaswa kuwa wepesi na karibu na wananchi kila mahali ili kushughulikia kero zao kwa haraka na kuwapa majibu mazuri,”alisema Makalla.

Alisema zipo tabia za baadhi ya watendaji wa serikali ambao hutoa vitisho kwa wananchi hivyo waache tabia hiyo na badala yake wafanye ofisi za serikali kimbilio la wananchi ikiwemo kupunguza urasimu na lugha za maudhi kwa wananchi.

Katika hatua nyingine ameuagiza Uongozi wa jiji la Mbeya kurejesha maeneo yote waliogawa kwa raia wa kigeni ili taratibu zifuatwe na yarejeshwe kwa wananchi kwa ajili ya soko.

Pia ameagiza wananchi 36 waliotapeliwa  mashamba yao na mwekezaji warejeshewe baada ya mwekezaji kutokujenga Shule kwa miaka 14 kama alivyoahidi.

Aidha amewaagiza TRA kuweka utaratibu wa kwenda kwenye Kata kukusanya kodi ya majengo badala ya kuwapa usumbufu wananchi kwenda kuweka foleni ofisi za TRA.
Posted by MROKI On Wednesday, March 22, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo