Nafasi Ya Matangazo

March 28, 2017

Kaimu Mkuu wa wilaya ya Kasulu ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Kanali Marko Gaguti akiongoza oparesheni hiyo ya kutokomeza mashamba ya dawa za kulevya.
 Baadhi ya watuhumiwa wakiwa chini ya ulinzi.
Na Rhoda Ezekiel,Kigoma
KAMATI ya  Ulinzi na Usalama Wilayani Kasulu, Mkoani Kigoma imeteketeza Shamba la bangi hekari moja  iliyo kuwa imelimwa katika hifadhi ya pori la Akiba  Makere Kusini, wilayani humo na kukamata watuhumiwa wanne.

Miongoni mwa watuhumiwa hao wawili ni raia wa nchi jirani ya Burundi waliokuwa wakifanya kazi katika shambaa hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari  Kaimu Mkuu wa wilaya ya Kasulu ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Kanali Marko Gaguti wakati wa kuteketeza shamba hilo alisema kumekuwa na tabia ya wakulima wengi kulima bhangi pembezoni mwa mji wakichanganya na mazao Mengine suala linalopelekea watoto wengi kuharibika na uhalifu kuongezeka.

Gaguti alisema  baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Wananchi kwamba kuna mtu analima bangi jeshi la polisi kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ilifanya msako na kukamata shamba la  Mkulima, Yotham Ngeze aliekuwa akiwatumia vibarua wanne wakiwemo warundi wawili na vijana wawili ambao walikuwa wakilima shamba hilo.

Aidha Gaguti aliwataka wakulima kuacha tabia ya kulima bhangi zao ambalo ni haramu na badala yake watumie aridhi nzuri waliyo nayo kulima mazao ya chakula kutokana na hali ya upatikanaji wa chakula ulivyo kwa sasa, na kwa atakae kutwa analima zao hilo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake Serikali inamacho mengi wataendelea kuwafuatilia popote pale .

Pia Mkuu huyo aliwataka Wakulima kuacha tabia ya kuwatumia wahamiaji haramu katika mashamba yao hali inayo sababisha Migogoro ya Wakulima kuongezeka kutokana na ugomvi unaotokea baada ya kuwatumia vibarua hao na kuacha kuwalipa, kulikuwa na kesi nyingi za raia kutoka Burundi kuwauwa watanzania kwa kuwalipizia kisasi baada ya kuwatumia bila malipo.

"Niwaombe wakulima Muachane na tabia ya kuja kulima bhangi katika hifadhi zetu za misitu uhalifu umekuwa ukiongezeka kila siku ni kutokana na Vijana wanapo tumia madawa ya kulevya wengi wao huishia kufanya uhalifu na wengine kushindwa kuendelea na masomo hatutavumilia watoto wetu na Wananchi waendelee kuteseka tutakae Mkamata atalipa faini na kifungo pia",alisema Gaguti.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, DCP Fredinandi Mtui alisema kwa Kipindi cha mwezi huu wamekamata hekari saba za bangi na watuhumiwa nane, ambapo hekari sita ziliteketezwa katika Wilaya ya Kakonko na hekari moja katika Wilaya ya Kasulu na jeshi la polisi linaendelea na kuwasaka wote wanao lima na kutumia bhangi ilikuweza kukomesha madawa ya kulevya.

Nae Mmiliki wa shamba la bangi katika msitu wa hifadhi Makere Yotham Ngeze alikili kulima zao hilo na kwamba analima kwaajili ya matumizi yake binafsi na kwamba anapo tumia bhangi anajikuta anafanya kazi kubwa sana ya kulima kwa siku anaweza kulima nusu heka akiwa amwtumia zao hili.

Alisema alianza kutumia bhangi tangu mwaka 1973 akiwa katika Mashamba ya Mikonge Mkoani tabora na amekuwa akilima zao hilo liweze kumsaidia kupata bangi kwa urahisi kutokana na mazoea aliyo jiwekea tangu akiwa kijana hawezi kuishi bila bhangi.

Nao baadhi ya vijana waliokuwa wakimlimi0a mzee huyo akiwemo Simoni Ndayahimana raia wa Burundi wamejikuta wakianza matumizi ya bangi baada ya kulima katika shamba hilo hali inayopelekea vijana wengi kupoteza nguvu kazi kutokana na matumizi na ulimaji wa madawa ya kulevya.
Posted by MROKI On Tuesday, March 28, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo