Nafasi Ya Matangazo

March 24, 2017



Rais Dkt John Pombe Magufuli akipokea hati ya utambulisho kutoka kwa Mhe. Laszlo Eduard Mathe Balozi wa Hungary nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi Kenya leo Machi 23, 2017 Ikulu jijini Dar es salaam.
 ************
Balozi wa Hungary hapa nchini mwenye makazi yake Nairobi, Kenya,Lazaro Eduard Mathe amemhakikishia Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwa nchi yake ipo tayari kushirikiana na Tanzania katika kuendeleza sekta ya viwanda na kwamba wawekezaji kutoka Hungary wameanza kufanya mchakato wa kujenga kiwanda cha kuunda mabasi ya abiria.

Lazaro Eduard Mathe amesema hayo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na Rais Magufuli muda mfupi baada ya kukabidhi hati zake za utambulisho akiwa ni miongoni mwa Mabalozi sita waliokabidhi hati hizo.

Pamoja na nia ya kujenga kiwanda cha kuunda mabasi ya abiria,  Lazaro Eduard Mathe amempongeza Rais Magufuli kwa juhudi kubwa anazofanya kujenga uchumi wa Tanzania na ameahidi kuwa Hungary itakuza na kuimarisha ushirikiano wake na Tanzania kwa kuleta teknolojia katika sekta mbalimbali ikiwemo viwanda na kilimo pamoja na kuwahimiza wawekezaji kuja kuwekeza nchini Tanzania.
 
  Rais Dkt John Pombe Magufuli akipokea hati ya utambulisho kutoka kwa Dmitry Kuptel Balozi wa Mauritius  nchini mwenye makazi yake jijini Maputo nchini Msumbiji leo Machi 23, 2017 Ikulu jijini Dar es salaam.

Rais  Dkt John Pombe Magufuli akipokea hati ya utambulisho kutoka kwa Mhe. Sidibe Fatoumata Kama, Balozi wa Guinea  nchini mwenye makazi yake jijini Addis Ababa, Ethiopia, leo Machi 23, 2017 Ikulu jijini Dar es salaam.

Rais Dkt John Pombe Magufuli akipokea hati ya utambulisho kutoka kwa Lebonaamang Thanda Mokalake, Balozi wa Botswana nchini mwenye makazi yake jijini Lusaka, Zambia, leo Machi 23, 2017 Ikulu jijini Dar es salaam.

 Rais Dkt John Pombe Magufuli akipokea hati ya utambulisho kutoka kwa Mhe. Adam Maiga ZakariaouBalozi wa Niger  nchini mwenye makazi yake jijini Addis Ababa, Ethiopia, leo Machi 23, 2017 Ikulu jijini Dar es salaam.

Rais Dkt John Pombe Magufuli akipokea hati ya utambulisho kutoka kwa  Mhe. Jean Pierre Jhumun,  Balozi wa Belarus  nchini mwenye makazi yake jijini Addis Ababa Ethiopia  leo Machi 23, 2017 Ikulu jijini Dar es salaam.
*************
Aidha, Rais Magufuli amepokea hati za utambulisho za Balozi wa Belarus hapa nchini mwenye makazi yake Mjini Addis Ababa - Ethiopia, Dmitry Kuptel ambaye amemhakikishia kuwa katika kuimarisha uhusiano na ushirikiano, nchi hiyo imejipanga kuimarisha uwepo wake barani Afrika kwa kuongeza uwekezaji katika viwanda na biashara.
Mabalozi wengine waliowasilisha hati zao za utambulisho ni Fatoumata Kaba Sidibe, Balozi wa Guinea hapa nchini mwenye makazi yake Mjini Addis Ababa - Ethiopia, Balozi wa Botswana hapa nchini mwenye makazi yake Mjini Lusaka – Zambia , Lebonaamang Thanda Mokalake, Balozi wa Niger hapa nchini mwenye makazi yake Mjini Addis Ababa – Ethiopia, Adam Maiga Zakariaou na Balozi wa Mauritius hapa nchini mwenye makazi yake Mjini Maputo – Msumbiji , Jean Pierre Jhumun.

Rais Magufuli amewapongeza Mabalozi wote walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini na amewahakikishia kuwa Tanzania itaendeleza na kuimarisha zaidi uhusiano na nchi hizo huku akiwasihi Mabalozi hao kutilia mkazo uhusiano na ushirikiano katika kiuchumi.

“Nimeambiwa Mauritius inafanya vizuri katika viwanda vya nguo na uzalishaji wa sukari, nitafurahi sana kuona wawekezaji wa kutoka Mauritius wanakuja kuzalisha sukari hapa nchini, nakuomba Mhe. Balozi ukampe ujumbe Mhe. Rais kuwa ninawakaribisha sana wawekezaji wa kutoka Mauritius” amesema Rais Magufuli.
Posted by MROKI On Friday, March 24, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo