Nafasi Ya Matangazo

October 21, 2016

1
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ,Hamad Masauni, akikata utepe kuashira ufunguzi wa kituo kipya cha kisasa cha huduma ya magari madogo na makubwa kilichopo Magomeni Mwembe chai jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Superdoll Tanzania ,Seif .A. Seif, Kushoto ni Kamanda wa kikosi cha Usalama Barabarani ,Mohamed Mpinga na Meneja usambazaji kanda ya Afrika Mashariki Dkt.Fulgence Bube.
2
Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Superdoll Tanzania ,Seif .A. Seif, akimsikiliza kwa makini,Naibu waziri wa mambo ya Ndani ,Mhandisi Hamad Masauni katika hafla ya uzinduzi wa kituo kipya cha kutoa huduma kwa magari makubwa na madogo kilichopo Magomeni Mwembe Chai jijini Dar es Salaam.
3
Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Superdoll Tanzania ,Seif .A. Seif, akizungumza na wadau waliofika katika uzinduzi wa kituo kipya cha huduma kwa wateja.
5
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ,Mhandis Hamad Masauni, akizungumza na wadau waliofika katika uzinduzi wa kituo cha wateja.
dsc_0149
dsc_0145
dsc_0137
Wadau wa mbalimbali wakifuatilia uzinduzi.
6
Msimamizi wa kituo cha kutoa huduma za magari cha Mwembechai akitoa maelezo kwa waziri na viongzi mbalimbali.
11
Wafanyakazi wa Kampuni ya Superdoll wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa kituo cha kisasa cha kutoa huduma ya magari makubwa na madogo kilichopo Magomeni mwembe chai jijini Dar es Salaam.
************
Watanzania wanaotumia vyombo vya moto wametakiwa kufanya uchunguzi wa mara kwa mara kabla ya kuanza safari ili kuweza kupunguza ajali za barabarani.

Hayo ameyasema Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Ahamad Masauni wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Kisasa cha kutoa huduma ya magari makubwa na madogo, amesema kuwa kufanya uchunguzi wa magari katika kituo hicho kitasaidia kupunguza ajali barabarani.

Amesema teknolojia inakua kwa kasi hivyo magari ya sasa yanatakiwa kufanyiwa uchunguzi wa kisasa kabla ya kuanza kwa safari katika kituo cha mwembe chai.

Masauni amesema Superdoll wamekuwa wabunifu wa teknolojia ya kisasa ya katika vyombo vya moto ikiwa ni kuweka safari kuwa salama kwa safari zote.

Amesema kuwa kunzisha kituo hicho watakuwa wamesaidia ujenzi katika masuala ya usalama barabani na kuweza kupunguza ajali za barabarani.

Masauni amesema kuwa watashirikiana na superdoll na kampuni ya matairi ya Michelin katika kufanya uchunguzi wa magari kwa teknolojia ya kisasa

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabani, Naibu Kamishina wa Jeshi la Polisi, Ahmed Mpinga amesema superdoll wamekuwa wadau wa usalama barabarani na kuendelea kuwa wabunifu katika teknolojia mbalimbali.

Amesema wanaomiliki vyombo vya moto watumie kituo cha uchunguzi wa teknolojia ya katika kuweza usalama wa gari na maisha watu katika kufikia lengo la serikali ya kupunguza ajali barabarani.

Mkurugenzi wa Superdoll, Seif Seif amesema kuwa kuna tayari zimekuwa zikiingizwa nchini ambazo matumizi yake ni kwa nchi zenye barafu wakati Tanzania hatuna uhitaji wa hizo.
Posted by MROKI On Friday, October 21, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo