Nafasi Ya Matangazo

September 27, 2016



SHIRIKA la ndege la Precision Air, limerudisha rasmi safari zake za kuelekea HAHAYA – nchini Comoro kuanzia leo tarehe 27 Septemba 2016. Ndege kuelekea komoro iliondoka saa 4 asubuhi kuelkea HAHAYA na ilitarajiwa kuwasili huko saa 5 Asubuhi. 

Precision Air ilisitisha safari hizo mnamo mwaka 2014 na kutangaza kuzirejesha mapema mwezi  Agosti mwaka huu.

Akizungumzia kurejeshwa kwa safari hizo Mkurugenzi wa Biashara wa shirika hilo Bw. Robert Owusu amesema kuwa Precision Air imejipanga kutoa huduma ya uhakika ya usafiri wa anga kati ya Tanzania na Comoro, ambayo itarahisisha biashara na safari kati ya nchi hizo.

“Safari zetu zitakua kila siku ya Jumanne, Alhamisi na Jumamosi. Na ratiba hii imepangwa makhususi kukidhi mahitaji ya safari za Kiserekali, Kibiashara na hata zile za mapumziko na  kulingana na mapokeo ya soko tunatarajia kuongeza safari zaidi.” Bw. Owusu amedokeza.

 “Tunafuraha kurudisha safari hizi kama tulivyo ahidi , nah ii itakua sehemu ya 13 katika mtandao wetu kwa ujumla na ni ya pili kwa safari zetu za kikanda. Nimatazamio yetu kutengeneza mtandao wa safari ambao utawawezesha abiria wetu kuunganisha safari zao ndani ya Afrika Mashariki, Africa na Duniani kwa ujumla. 

Tunajivunia kuwa na mtandao bora ziaidi unaowapa wateja urahisi wa kuunganisha safari zao na hatutachoka kuuboresha kuhakikisha tunaendana na matakwa ya soko.” Bw. Owusu amefafanua zaidi.

Precision air ndilo shirika pekee la Kitanzania lilo chini ya umoja wa Mashirika ya Ndege Duniani IATA na hivyo huwawezesha abiria kufanya booking zao na kuunganisha na mashirika mengine ya Kimataifa. 

Kwa safari za ndani Precision Air inasafiri kwenda sehemu 13 ikitokea Dar es Salaam kuelekea Arusha, Kilimanjaro, Mwanza, Bukoba, Musoma, Tabora, Kigoma, Mtwara, Zanzibar and Pemba.
Posted by MROKI On Tuesday, September 27, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo