Nafasi Ya Matangazo

June 28, 2016

Mshambuliaji wa Timu ya TP Mazembe, Mtanzania Thomas Ulimwengu akichuana vikali na Beki wa Yanga, Kelvin Yondani, katika Mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika, uliopigwa jioni hii kwenye Uwanja wa TAifa jijini Dar es salaam. Yanga imelala kwa bao 1-0. Matokeo hayo sasa Yanga inashika mkia katika kundi hilo ikiwa imepoteza mechi zote mbili huku TP Mazembe ikiongoza kundi A ikiwa na Point 6 na magoli 4. 
 Mshambuliaji wa timu ya Yanga,Obrey Chirwa akiichambua ngome ya timu ya TP Mazembe, katika mtanange uliopigwa jioni hii kwenye dimba la Taifa (Uwanja wa Taifa) Jijini Dar es salaam, ikiwa ni Mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika. Hadi kupanga cha mwisho kinalia, Yanga wamelala kwa bao 1-0.
Beki wa TP Mazembe, Christian Nekadio akiruka juu kuondosha hatari iliyoelekezwa langoni kwake na Mshambuliaji wa Yanga, Juma Hassan Mahadhi.
Kipa wa Yanga,Deogratius Munish 'dida' akinyaka mpira kwa umaridadi.
Posted by MROKI On Tuesday, June 28, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo