Nafasi Ya Matangazo

June 28, 2016

 Meya wa Manispaa ya Ilala, Jijini Dar es Salaam, Charles Kuyeko akimtwisha ndoo ya maji Mkazi wa Mtakuja Kata ya vingunguti baada ya kuzindua mradi wa maji safi na salama katika kata hiyo leo. 
Meya wa Manispaa ya Ilala, Jijini Dar es Salaam, Charles Kuyeko (kulia) akisaini kitabu cha wageni katika Kata ya vingunguti alipokwenda kuzindua mradi wa maji na vyoo katika Kata hiyo leo. Pamojane ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Kata ya Vingunguti, Omary Kumbilamoto.
MEYA wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko amezindua mradi wa maji na vyoo viwili vya kulipa katika Kata ya Vingunguti Manispaa ya Ilala, Jijini Dar es Salaam leo.

Uzinduzi wa miradi hiyo ni jitihada za Manispaa Katika kuonyesha dhamira ya kutatua kero sugu za wananchi wa Halmashauri ya Manispaa hiyo na viunga vyake.

Miradi hiyo miwili iliyojengwa katika Kata ya Vingunguti, mtaa wa Mtakuja na mtaa wa Mtambani imejengwa na CIUP chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia.

Awali akizungumza katika uzinduzi huo Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Mtakuja,  Sharifu Abdallah Mbulu alisema kuwa miradi hiyo ilikuwa ijengwe na kukamiliki toka mwaka 2013 lakini kutokana ubadhirifu na usimamizi mbovu wa uongozi uliopita walishindwa kusimamia ujenzi wa miradi hiyo na kukamilika kwa wakati. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Uongozi mpya wa mtaa wa mtakuja uliongia mwaka 2014 kwa kushirikiana na Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Vingunguti, Omary Kumbilamoto kwa muda mfupi wamefanikiwa kuikamilisha miradi hiyo.

Naibu Meya na Diwani wa Vingunguti, Omary  Kumbilamoto akizungumza katika uzinduzi huo alisema mradi huo utakuwa na faida tatu ambapo  mradi wa Maji umelenga kuwaondolea wananchi wa mitaa adha ya Maji, kuboresha usafi wa mazingira kwani wananchi hasa wafanyabiashara walikuwa wanakojoa hadharani na kuelekea kuchafua mazingira na mapato ambayo yatapatikana kutokana na watu kulipa fedha.

Kumbilamoto alitumia nafasi hiyo kupiga marufuku uchafuzi wa mazingira hasa kukojoa hovyo kwani sasa hakuna kisingizio tena.

Alimweleza Mstahiki Meya wa Ilala kuwa Kata ya Vingunguti pia inakabiliwa na changamoto ya baadhi ya mitaa kutokuwa na maafisa watendaji. Kata inamitaa Sita lakini mitaa mitatu ndiyo ina maafisa watendaji na mitaa mitatu haina watendaji hali ambayo inarudisha nyuma utendaji kazi. Lakini changamoto nyingine ni kufufua visima vya Maji katika mitaa minne iliyobakia ya Kata hiyo.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ndiye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo , Charles Kuyeko akizungumza katika uzinduzi huo amempongeza Diwani wa Kata ya Vingunguti na viongozi wenzake wa mitaa yote ya Kata hiyo.

Kuyeko amewapongeza pia wananchi wa Kata ya Vingunguti kwa kuchagua viongozi wachapakazi na wenye shauku ya kuwaletea maendeleo wananchi wao na kusemafaida ya kutumia vizuri haki ya kupiga kura ni kuchagua kiongozi bora ambaye ni mwakilishi wa wananchi na mwenye uwezo wa kutatua kero za wananchi wake ambapo Vingunguti mmefanikiwa.

“Vingunguti ninaijua vizuri sana, lakini Vingunguti ninayoijua siku zote siyo hii ya leo, imebadilika sana imekuwa safi na hata nyuso za watu wake zimebadilika, zinaonyesha matumaini mazuri tofauti na zamani,” alisema Kuyeko.

Aidha,  Kuyeko aliwataka wananchi wa Kata ya Vingunguti bila kujali itikadi zao watoe ushirikiano wa dhati kwa Diwani kwani nimchapakazi na mpenda maendeleo.

“Diwani wenu ni Naibu Meya wa Ilala hivyo kiitifaki ni msaidizi wangu mkuu kwa nafasi hiyo nimepata fursa ya kumfamu vizuri ni mchapakazi, mpenda maendeleo kwa hiyo mkimpa ushirikiano mzuri maendeleo mnayoyataka mtayapata,” alisema Kuyeko.

Meya pia ametumia nafasi kuwataka Madiwani wote wa Ilala kuiga mfano wa Diwani wa Vingunguti kuwa karibu na wananchi wao ili kujua changamoto zinazowakabili. Kuyeko amewataka Madiwani kushirikiana na wananchi wa Kata zao kubuni miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi wao.

“Wapiga kura wanamatumaini na sisi, maana wakati tunaomba kura tuliahidi Mabadiliko, Mabadiliko hayo ni kuleta maendeleo kwa wananchi wetu,” alisema Kuyeko.

Kuyeko pia alisema kwa nafasi yake ya kuwa Meya wa Ilala kwa kushirikiana na Madiwani wote miradi ya maendeleo itafanikiwa.

Mstahiki Meya amechangia Tshs. 5,000,000/ ili zisaidie kusukuma miradi ya maendeleo kwa Kata ya Vingunguti hasa kufufua visima vya Maji kwa mitaa iliyobakia.


Uzinduo huo ulihudhuriwa na wananchi pamoja na viongozi wa Ukawa Kata ya Vingunguti. 
Posted by MROKI On Tuesday, June 28, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo