Nafasi Ya Matangazo

May 26, 2016

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, TPB, Be.Sabasaba Moshingi,(kushoto), akijibu baadhi ya hoja za wajumbe wa Mkutano wa mwaka wa wanahisa wa Benki hiyo jijini Dar end Salaam Leo Mei 25, 2016. 

Wajumbe walipokea taarifa ya uendeshaji Benki hiyo kwa mwaka 2015 ikiwa ni pamoja na mipango ya uendeshaji wa Benki kwa mwaka huu wa 2016. Pamoja na mambo mengine, Bw.Moshingi alisema benki inampango wa kuingia kwenye soko la his a(Dar es salaam stock exchange), sambamba na kuongeza Huduma za ATM kwenye matawi yake mbalimbali kote nchini. 

Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi, Profesa Lettice Rutashobya, na kulia in Katibu wa Bodi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Sheria wa Benki hiyo, Bi.Mystica Mapunda Ngongi.Wakichangia hoja mbalimbali baada ya kupokea taarifa ya mahesabu ya fedha iliyosomwa na Meneja wa kampuni ya ukaguzi wa mahesabu ya Nexia SJ Tanzania, Bw.Fulgensio Mgaya, ambaye alisema mahesabu ya Benki hiyo hayakukutwa na dosari, wajumbe wa mkutano huo, Bi.Theresia A Chitumbi na Bw. James Sando, wameupongeza uongozi wa Benki hiyo kwa usimamizi thabiti na uendeshaji mzuri wa Benki. 
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Benki ya Posta Tanzania, TPB, Profesa Lettice Rutashobya, (wapili kulia), akiendesha mkutano wa mwaka wa wanahisa wa benki hiyo, jijini Dar es Salaam Mei 25, 2016. Kikao hicho kimejadili utendaji kazi wa benki katika mwaka wa 2015/2016 ambapo wajumbe walijadili mapato ya benki, upanuzi wa huduma za kibenki nchini ikiwa ni pamoja na mabporesho ya huduma kwa wateja. Wengine pichani kutoka kulia, ni Msajili wa Hazina, Bw. Lawrence Mafuru, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar, Bw. Hamisi Mussa Omar. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Mwenyekiti akiendesha kikao cha wanahisa wa TPB.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Benki ya Posta Tanzania, TPB, Profesa Lettice Rutashobya, (wapili kulia), akiendesha mkutano wa mwaka wa wanahisa wa benki hiyo, jijini Dar es Salaam Mei 25, 2016. Kikao hicho kimejadili utendaji kazi wa benki katika mwaka wa 2015/2016 ambapo wajumbe walijadili mapato ya benki, upanuzi wa huduma za kibenki nchini ikiwa ni pamoja na mabporesho ya huduma kwa wateja. Wengine pichani kutoka kulia, ni Msajili wa Hazina, Bw. Lawrence Mafakizungumza kwenye mkutano huo
 Wakurugenzi wa idara mbalimbali za TPB, wakibadilishana mawazo wakati wa mapumziko
 Katibu Mkuu wizara ya fedha serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bw.Hamisi Mussa Omar(kulia), na Mkurugenzi wa sheria na Katibu wa Bodi ya TPB, Bi.Mystica Mapunda Ngongi.
 Picha ya pamoja ya uongozi wa TPB, na wanahisa waliohudhuria mkutano huo
 Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Bw. Sa asaba Moshingi, akipitia makabrasha
 Katibu Mkuu wizara ya fedha, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bw.Hamisi Mussa Omar. (kulia), akizungumza kwenye mkutano huo. Kushoto ni Bw.James Sando wa TPC.
 Msajili wa Hazina kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Lawrence Mafuru, (kushoto), akiteta jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Bw. Sabasaba Moshingi
Mwenyekiti wa Bodi ya TPB, Profesa Lettice Rutashobya, (kulia), akifurahia jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Bw. Sabasaba Moshingi
Posted by MROKI On Thursday, May 26, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo