Nafasi Ya Matangazo

May 25, 2016

 Mkurugenzi wa kampuni ya  Darbrew Limited inayotengeneza Chibuku,David Cason  akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Darbrew. 
 Wafanyakazi wa Kampuni ya Darbrew wakifurahia tuzo hiyo. 
 Mkurugenzi wa kampuni ya  Darbrew Limited inayotengeneza Chibuku,David Cason  akikabidhi tuzio hiyo kwa mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo. 
 Wafanyakazi wakiwa katika tafrija 
 Mkurugenzi wa kampuni ya  Darbrew Limited inayotengeneza Chibuku,David Cason  akijadiliana jambo na viongozi wa kampuni hiyo. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI. 

Mkurugenzi wa kampuni ya  Darbrew Limited inayotengeneza Chibuku,David Cason  akiongea na wafanyakazi wakati ya hafla ya kusherehekea kushinda  tuzo ya uendelezaji vinywaji vya asili kutoka SABMiller  iliyofanyika kiwandani hapo jana
******************
KAMPUNI ya Darbrew inayotengeneza pombe ya Chibuku imetunukiwa tuzo kutoka SABMiller  ya uendelezaji vinywaji vya asili nchini katika kongamano la masoko la viwanda  lililofanyika mjini Cape Town nchini Afrika ya Kusini.

Darbrew iliyopo chini ya TBL Group iliibuka kidedea baada ya kushindanishwa na viwanda vinavyotengeneza vinywaji vya kienyeji vilivyopo chini ya SABMiller vilivyopo katika nchi za Botswana,Malawi na Uganda.

Akitangaza mafanikio hayo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana,Mkurugenzi Mkuu wa Darbrew, David Cason alisema kuwa tuzo hiyo ni mafanikio makubwa kwa kampuni na aliwapongeza wafanyakazi wote kwa kujituma na kuhakikisha yanapatikana mafanikio siku hadi siku.

“Tuzo hii sio ya mtu mmoja imepatikana kutokana na mchango wa kila mfanyakazi wa DarBrew na inabidi kuongeza bidii zaidi katika kazi ili mafanikio zaidi yapatikane na kampuni izidi kusonga mbele na kuwa miongoni mwa makampuni makubwa ya vinywaji katika ukanda huu wa Afrika Mashariki”.Alisema Cason.

Alisema hatua ya kampuni kushindanishwa na viwanda vikubwa na kuibuka na tuzo ni jambo la kujivunia kila mfanyakazi  na aliwashukuru mawakala na wateja wote wa Chibuku kwa kuunga mkono biashara ya kampuni.

Kwa upande wake Meneja wa Mauzo wa DarBrew,Freddy Kazindongo alisema aliwapongeza wafanyakazi na kuwashukuru wateja kwa mafanikio yaliyopatikana na kuongeza kuwa kampuni imejizatiti kuongeza zaidi ubora wa huduma za uzalishaji na usambazaji na kuhakikisha kinywaji cha Chibuku kinawafikia wananchi popote walipo na wanakipata kulingana na kila mtu na uwezo wake .

Katika kuthibitisha hilo alisema wiki hii kampuni imezindua chibuku super ya mililita 750 ambayo itawawezesha wateja kupata  kinywaji  hicho kwa gharama nafuu.

Kazindogo alisema mkakati wa kampuni ni kuhakikisha  urasimishaji wa pombe za kienyeji unafanikiwa ambapo wananchi wataweza kupata kinywaji cha asili katika mazingira bora ya usafi wakati huohuo wakikinunua wanachanga pato la serikali kwa njia ya kodi kitu ambacho hakipo kwa pombe nyingine za asili.


Pia alisema kuwa kampuni itazidi kupanua wigo wa ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja  ambazo zinawawezesha mawakala wakubwa na wadogo na akina mama wanaouza pombe za asili kujipatia mapato ya uendesha maisha vilevile kupunguza uharibifu wa mazingira kutokana na akina mama waliokuwa wanapika pombe za asili kwa kutumia kuni na mkaa watakuwa wanauza pombe ambayo tayari imetengenezwa badala ya kutumia muda mwingi kutengeneza pombe.
Posted by MROKI On Wednesday, May 25, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo