Nafasi Ya Matangazo

April 28, 2016





Mkuu wa kitengo cha elimu kwa Umma kitengo cha Usalama barabarani makao makuu ya Polisi ASP,Abel Swai akitoa mada kwa wafanyakaziwa kampuni ya TBL jijini Dar es Salaam wakati wa semina ya masuala ya usalama wakati kuadhimisha  Siku ya Afya na Usalama Duniani.Semina hiyo ilifanyika kiwanda cha TBL cha Ilala.


Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL wakisikiliza mada wakati wa semina ya usalama kazini wakati wa maadhimisho ya siku ya Afya na Usalama Duniani

 Mmoja wa wafanyakazi wa TBL akiuliza swali wakati wa semina ya usalama kazini wakati wa maadhimisho ya siku ya Afya na Usalama Duniani iliyofanyika kiwanda cha ilala jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu wa masuala ya afya na jamii Lilian Msaki,akitoa elimu kwa wafanyakazi wa TBL wakati wa semina ya usalama kazini wakati wa maadhimisho ya siku ya Afya na Usalama Duniani iliyofanyika kiwanda cha ilala jijini Dar es Salaam. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.

Maofisa wa Jeshi la Polisi na TBL wakibadilisha mawazo  muda mfupi baada ya kumalizika kwa semina semina ya usalama kazini wakati wa maadhimisho ya siku ya Afya na Usalama Duniani iliyofanyika kiwanda cha ilala jijini Dar es Salaam.
 *************************

Wafanyakazi wa kampuni ya TBL Group na wanajamii wote wameaswa kuzingatia kanuni za usalama na kuzitekeleza  wakati wote ili kuepuka uwezekano wa kupata majanga ambayo yanaweza kuepukika .

Wito huo umetolewa na Meneja anayesimamia mazingira ya sehemu za kazi na Usalama wa  kiwanda cha TBL Group ,Renatus Nyanda wakati akihojiwa kuhusiana na maadhimisho ya Siku ya Usalama Kazini Duniani ambayo imeadhimishwa na kampuni hiyo kwa kushirikisha wafanyakazi wake wote .

Nyanda alisema kuwa linapozungumziwa suala la usalama mahali pa kazi wengi wamekuwa wakidhani kuwa unapaswa kuzingatia kanuni za usalama unapokuwa kazini tu,dhana ambayo alidai kuwa ni potofu kwa kuwa Usalama unapaswa kuzingatia wakati wote na mahali popote na kuwa suala la usalama linamhusu kila mtu awe mfanyakazi waofisini,kiwandani, mkulima, mfanyabiashara na shughuli nyinginezo.

Alisema kampuni ya TBL Group imekuwa ikilipa kipaumbele suala la usalama kwa wafanyakazi wake ambapo tayari imefanikiwa  kupunguza matukio ya ajali  kazini kwa wafanyakazi wake kutokana na utekelezaji wa mpango wa tahadhari za kiafya na usalama wa kampuni mama ya SABMiller ambao umefanyiwa utafiti wa kina na wenye kutoa maelekezo ya kuepusha ajali sehemu kazini na maeneo mengine mbali na kazini.

Alisema elimu hii  ya tahadhari na usalama ambayo imekuwa ikitolewa mara kwa mara na kutekelezwa kwa vitendo haiwasaidii wafanyakazi wanapokuwa kazini tu bali hata wawapo majumbani kwao au sehemu yoyote nyingine wakiitumia itawasaidia  kuwaepusha na majanga mbalimbali ambayo yamekuwa yakijitokeza katika shughuli za maisha ya kila siku.

“Programu hii inayojulikana kama Safety around Bevarage inafundisha masuala  mengi kuhusiana na usalama kazini ambapo tangu ianze kutekelezwa na kampuni ya TBL Group imeanza kuonyesha mafanikio katika  ofisi na viwanda vyake vyote kwa kuwa ni nadra matukio ya ajali kujitokeza kwa wafanyakazi na wageni wanaotembelea kampuni na taasisi nyingi zinavutiwa kuja kwenye kampuni yetu kujifunza masuala ya usalama”.Alisema

Katika kuadhimisha siku hii wafanyakazi walishiriki semina zinazohusiana na masuala ya usalama zilizotolewa na serikali kupitia jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani pia wataalamu wa masuala ya bima na Afya ya jamii walitoa mada kuhusiana na umuhimu wa kuwa na bima.

Maadhimisho ya siku ya Usalama kazini Duniani huadhimishwa Aprili 28 kila mwaka  ambapo kampeni za kuhamasisha usalama mahali pa kazi hufanywa na taasisi mbalimbali duniani kote.
Posted by MROKI On Thursday, April 28, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo