Nafasi Ya Matangazo

April 25, 2016

Katibu Tawala Mpya wa Mkoa wa Simiyu, Jumanne Abdallah Sagini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 25 Aprili, 2016 amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara.
Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa kati ya Makatibu tawala hao 10 ni wapya, 2 wamebadilishiwa vituo vya kazi na 13 wamebakisha katika vituo vyao vya sasa.

Makatibu Tawala wapya walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
    1.      Arusha -                      Richard Kwitega
    2.     Geita -                         Selestine Muhochi Gesimba
    3.      Kagera -                      Armatus C. Msole
    4.      Kilimanjaro -              Eng. Aisha Amour
    5.      Pwani -                        Zuberi Mhina Samataba
    6.      Shinyanga -                 Albert Gabriel Msovela
     7.      Singida -                      Dr. Angelina Mageni Lutambi
    8.      Simiyu -                      Jumanne Abdallah Sagini
    9.      Tabora -                      Dkt. Thea Medard Ntara
    10.  Tanga -                        Eng. Zena Said

Makatibu Tawala waliobadilishwa vituo vya kazi ni kama ifuatavyo;
       1.      Kigoma -                     Charles Amos Pallangyo (Kutoka Mkoa wa Geita)
       2.      Morogoro -                 Dkt. John S. Ndunguru (Kutoka Mkoa wa Kigoma)


 Makatibu Tawala waliobakishwa katika vituo vyao vya sasa vya kazi ni kama ifuatavyo;
     1.      Dar es salaam -           Theresia Louis Mbando
     2.      Dodoma -                   Rehema Hussein Madenge
     3.      Iringa -                        Wamoja Ayubu Dickolagwa
     4.      Katavi -                        CP Paul Chagonja
     5.      Lindi -                         Ramadhan Habibu Kaswa
     6.      Mara -                         Benedict Richard Ole Kuyan
      7.      Manyara -                    Eliakimu Chacha Maswi
      8.      Mbeya-                        Mariam Amri Mjunguja
     9.      Mtwara -                      Alfred Cosmas Luanda
    10.  Mwanza -                    CP. Clodwing Mathew Mtweve
     11.  Njombe -                    Jackson Lesika Saitabau
     12.  Rukwa -                       Symthies Emmanuel Pangisa
    13.  Ruvuma -                    Hassan Mpali Bendeyeko
  Makatibu Tawala wa Mikoa 10 ambao wameteuliwa kwa mara ya kwanza,     wataapishwa siku ya Jumatano tarehe 27 Aprili, 2016 saa tatu asubuhi Ikulu Jijini Dar es salaam.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam

25 Aprili, 2016 
Posted by MROKI On Monday, April 25, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo