Nafasi Ya Matangazo

February 09, 2016

Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru (katikati), akikata tepe kikiwa ni ishara ya uzinduzi wa huduma za kifedha kwenye tawi la Benki ya Posta Babati mkoani Manyara leo Februari 9, 2016. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Sabasaba Moshingi, na kushoto ni Menyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi YA tpb, Profesa Lettice Rutashobya.


Msajili wa hazina, Lawrence Mafuru (wapili kushoto), akimpa zawadi mmoja wa wateja wa Benki ya Posta tawi la Babati, Theofil Muhale Tsaghayo baada ya kufungua rasmi huduma za kibenki katika tawi la Babati, mkoaniManyara Februari 9, 2016. kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo Prof. Lettice Rutashobya.
***************
Na Mwandishi wa K-VIS MEDIA, Babati
Benki ya Posta Tanzania (TPB) imezindua huduma za Kibenki kwa kufungua tawi lake jipya kwenye mji wa Babati mkoani Manyara. Akizungumza kwenye uzinduzi huo Februari 9, 2016, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TPB, Lettice Rutashobya alisema tawi lililokuwepo hapo awali halikuweza kutosheleza mahitaji ya wakazi wa Mji wa Babati na vitongoji vyake kutokana na udogo wake.

‘’Tawi hili limefunguliwa ili kutimiza dhamira ya Benki yetu ya kupeleka huduma za kibenki karibu zaidi na wateja wake, na sasa Tawi hili litatoa huduma bora na za kisasa ikiwemo ile ya ATM kwa wafanyabiashara, wafanyakazi na wananchi kwa ujumla katika wilaya hii ya Babati”, aliwahakikishia Profesa Rutashobya.

Profesa Rutashobya aliwashukuru wateja wa TPB wa Wilaya ya Babati na vitongoji vyake kwa kutumia huduma wa TPB wa Wilaya ya Babati na vitongoji vyake kwa kutumia huduma za Benki hiyo kwa wingi, na kulifanya tawi hilo kuwa ni mojawapo ya matawi yanayofanya vizuri kifaida.

Naye Msajili wa Hazina, Lawrence N. Mafuru, ambaye ndiye aliyezindua huduma za kibenki za tawi hilo, aliipongeza Benki ya Posta kwa kuleta maendeleo ya kuninua maisha ya Mtanzania ya hali ya chini kwa kuongeza huduma za kibenki karibu na jamii hiyo, na kwa kubuni huduma mbalimbali hususan za mikopo, zenye lengo la kumuinua kimapata mwananchi wa chini.

Msajili huyo wa Hazina, alitumia nafasi hiyo kuwasisitiza wakazi wa Babati kuchangamkia fursa zinazotolewa na Benki ya Posta, kwa kufungua akaunti na kwenda kuomba mikopo ambayo oinatolewa kwa riba nafuu na benki hiyo.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi amesema uamuzi wa kujenga tawi hilo ambalo linatoa huduma zote zinapatikana kwenye matawi mengine ya Benki ya Posta Tanzania nchi nzima.


“Azma ya Benki ya Posta, ni kuwafikia na kutoa huduma za kibenki kwa wananchi wote (financial Inclusion), alisema Moshingi.

Posted by MROKI On Tuesday, February 09, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo