Nafasi Ya Matangazo

November 25, 2015

 Mkurugenzi Mstaafu wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dk. Felician Kilahama, akiwasilisha mada juu ya utafiti alioufanya maeneo mbalimbali nchini juu ya uhifadhi misitu.
 Washiriki wa semina hiyo ya siku moja wakifuatilia mada mbalimbali katika seimina hiyo Dar es Salaam jana.
***************

SERIKALI imetakiwa kuongeza nguvu katika uhifadhi na usimimamizi wa misutu nchini, ili kuendana na kasi ya matumizi ya Bidhaa za misutu kwa taifa.

Mkurugenzi Mstaafu wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dk. Felician Kilahama, alisema hali ya misutu ni mbaya na ipo haja ya serikali kuongeza nguvu katika utunzaji wa misutu hiyo kama inavyo fanya katika uhimizaji wa ukusanyaji mapato ya bidhaa za msitu.

“Misitu mingi iliyopo nchini, haina mpangio wa  usimamizi nchini ambao unaainisha ni bidhaa gani itavunwa wapi na kwa kipindi gani huku pakiwa na muelekeo unao onyesha makusanyanyo kutokana na usimamizi huo,”alisema Dk Kilahama. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Kilahama alisema misitu inafaida nyingi tofauti na inavyoonekana hivi sasa ya faida upande wa uvunaji magogo na uchomaji mkaa ambao huingiza fedha kwa njia ya ushuru na faini mbalimbali lakini misitu ndio chanzo cha mvua na upatikanaji wa maji na pia kukabiliana na hewa ukaa ambayo nitishio kwa sasa.

Aidha amesema kuwa lengo kuu la serikali kuanzisha wakala wa misitu nchini ni pamoja na kusimamia misitu ambayo ikisimamiwa vizuri italeta faida kubwa zaidi kuliko ukusanyaji fedha.

Mapema akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo  Mkurugenzi wa Shirika la AWF na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la kuhifadhi Misititu ya Asili Tanzania (TFCG),John Salehe alisema kuwa watanzania hivi sasa wanatakiwa wawe mstari wa mbele katika utunzaji wa misitu nchini na si kuiachia serikali pekee.

Salehe amesema ipo haja ya viongozi wa dini mbalimbali nchini wakatumiwa muda wao katika mahubiri yao kuelimisha waumini wao juu ya umuhimu wa utunzaji misitu.

“Misitu ya hifadhi ipo maeneo mengi nchini na miongoni mwa hiyo inazunguka katika vijiji vyetu, hivyo ipo haja ya viongozi wa dini kushirikiana na mamlaka husika kutoa elimu ya uhifadhi misitu katika kukabiliana na mabidiliko ya tabia nchi,”alisema Saleme.

Nae Afisa Misitu Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu na  Mratibu wa Misitu Asilia na mazingira asilia Tanzania, mradi, Gerald Kamwenda amesema wananchi wanatakiwa kubadili mtindo wao wa maisha ili kuokoa misitu nchini.

Tanzania inakabiliwa na matatizo ya tabia nchi lakini bado wananchi wanaendelea na uharibifu wa misitu hasa matumizi ya mkaa na kilimo cha kuhamahama.

“Tumegundua gesi ya kutosha hivyo wananchi wabadili matumizi kutoka kwenye mkaa hasa mijini na kutumia nishati ya gesi na umeme, vijijini wanachoma mkaa kwaajili ya kuiuza kwa watu wa mjini,”alisema Kamwenda.

 Washiriki wa semina hiyo ya siku moja wakifuatilia mada mbalimbali katika seimina hiyo Dar es Salaam jana.
Posted by MROKI On Wednesday, November 25, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo