Nafasi Ya Matangazo

November 25, 2015

Papa Francis akiwa na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya akiangalia burudani ya ngoma ya utamaduni mara tu alipowasili uwanja wa ndege wa kimatiafa wa jomo Kinyetta nchini Kenya leo.

 Papa Francis akizungumza jambo na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya baada ya kuwasili nchini humo ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya siku sita kwa nchi za Afrika za Kenya, Uganda na Jamhuri ya Afrika ya Kati,  huku Papa akitarajiwa  kueneza ujumbe wake wa Amani, maridhiano, mashauriano na kuchochea juhudi za kuzima migawanyiko. . Kushoto ni Mke wa Rais Kenyatta, Margaret Kenyatta na kulia ni Naibu Rais wa Kenya, William Ruto.

Afisa wa mawasiliano wa Vatican Padri Federico Lombardi alisema kwamba kwa Jorge Mario Bergoglio, ambalo ndilo jina kamili la Papa Francis, hii itakuwa ziara yake ya kwanza kabisa Afrika.

Hii ni ziara ya 11 ya Francis akiwa kama papa nje ya Vatican. Mapapa wawili wamewahi kuzuru mataifa haya kabla yake.
Posted by MROKI On Wednesday, November 25, 2015 1 comment

1 comment:

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo