Nafasi Ya Matangazo

November 25, 2015

Meneja Uhusiano wa Airtel, Bw Jackson Mmbando pamoja na Afisa Masoko Intaneti  wa Airtel , Eric Daniel wakionyesha huduma mpya ya Airtel Care itakayowawezesha wateja wa Airtel kudownload application na kupata huduma zote kwa urahisi kupitia simu zao .
************
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua application itakayowawezesha wateja wake  kupata huduma zote za Airtel kwa urahisi na kupitia application ijulikanayo kama  “Airtel care App”

Application  hii mpya ya “Airtel care App” ni moja kati ya huduma nyingi za kibunifu zinazotelewa na Airtel zenye lengo la kuwawezesha wateja  wa Airtel kutatua matatizo yao na mahitaji yao kwa urahisi wakati wowote

Akizungumza Wakati wa uzinduzi wa “Airtel care App” Meneja Uhusiano wa Airtel, Bw Jackson Mmbando alisema " Airtel tumejikita katika kutafuta, kujua mahitaji ya wateja wetu kwa lengo la kubuni bidhaa na huduma zinazokidhi na kutatua haja zao wakati wote.

“Airtel care App” inawawezesha wateja wetu, kuchagua kwa urahisi na kufanya mambo mengi zaidi katika simu zao ikiwemo kuongeza salio,  kuangalia salio, kuangalia matumizi na kiasi kilichosalia,  kununua vifurushi vya muda wa maongezi na intaneti,  kutuma na kupokea pesa, kununua mlio wa sauti, kupata ripoti ya miamala ya pesa uliyofanya pamoja na kupata msaada kwa watoa huduma. Huduma zote hizi zinapatikana kupitia application hiyo ya “Airtel care App”bila gharama yoyote ya ziada.

Ili kupata “Airtel care App” mteja anaweza kupakua au kudownload  Kupitia Google Play kwa simu aina ya Android na kwa simu Iphone wanaweza kupata huduma hii kwa kupakua au kudownload application kwenye Apple store.
Posted by MROKI On Wednesday, November 25, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo