Nafasi Ya Matangazo

October 02, 2015

Father Kidevu Blog, Kigoma 
Vijana Saba wa Jeshi la kujenga Taifa(JKT) kikosi cha 821 Bulombora wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma waliofariki katika ajali baada ya gari wallokuwa wakisafiria kupinduka jana huku wengine 22 wakijeruhiwa wametambulika.

Kamanda wa Jeshi la wananchi mkoa Kigoma, Kanali Mamdadi Kisui alisema kuwa wapiganaji hao walikumbwa na mauti hayo majira ya saa 10 jioni katika eneo la Mlima Pasua nje kidogo ya  Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Kanali Kisui alisema kuwa wapiganaji hao walikuwa wakisafiri na gari la Jeshi aina ya Iveco lenye namba za usajili 5717 JW 09 lililokuwa likitokea kambi ya Burombola kuelekea mjini Kigoma likiwa na jumla ya vijana 30 wa JKT.

Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Mkoa kigoma Maweni,Dk.Fadhili Kibaya aliwataja Askali waliofariki katika ajali hiyo kuwa Ally Kambagwa Mkazi wa Mtwara, Abeli Maisha Mkazi wa Morogoro, Eugini Bitati Mkazi wa Kibondo Mkoani Kigoma,  Saidi Sadara Mkazi Wa wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Bakari Kibaya Mkazi wa Tanga na Fredric Kaemela Mkazi wa Njiro mkoani Arusha.

Majeruhi wa Ajali hiyo ni:-  Benedict Ndokeye, Raphaeli Johanna, Athanasi Emanuel ,Abui Nzoge, Abubakari Piter, Abubakari Msubi, Deusi Manyanya, Edward Nyanda, Eliasi Magesa, Geofly Maliki, King Kasefu, Kamiliusi Agida, Lameki John, Maltini Kupatu, Stevin Denisi, Saidi Omary, Saidi Zuberi, Shabani Zakaria, Victer Saverxy, Jacksoni Nyarubu, Muhamed Nyimbo.

Miili ya marehemu imeagwa leo katika hospitali ya mkoa Kigoma na baadaye miili yao kusafirishwa kuelekea kwenye mikoa yao kwa mazishi ambapo Katibu Tawala wa mkoa Kigoma,Injia John Ngunguru aliongoza viongozi wa serikali na kamati ya ulinzi ya usalama kuaga na kuisindikiza miili hiyo akimwakilisha Mkuu wa mkoa Kigoma.
Posted by MROKI On Friday, October 02, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo