Nafasi Ya Matangazo

May 21, 2015

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza ameonekana akicheza mpira pamoja na marafiki zake mjini Bujumbura licha ya mgogora wa kisiasa nchini mwake.

Rais Nkurunziza,alikuwa akisakata kabumbu ndani ya mji mkuu wa Bujumbura mji uliokumbwa na maandamano makubwa tangu atangaze nia ya kuwania awamu ya tatu uongozini.

Hii leo habari kutoka Burundi zinasema kuwa mtu mmoja amepigwa risasi na kuuawa katika mji mkuu wa Bujumbura.

Mtu huyo alikuwa miongoni mwa waandamanaji wanaopinga hatua ya rais Pierre Nkurunziza kugombea urais kwa awamu ya tatu.

Walioshuhudia wanasema kuwa polisi walimpiga mwandamanaji huyo risasi mgongoni wakiwa katika eneo la Musaga linalotazamwa kama ngome ya upinzani.
Waandamanaji walijaribu kufika katikati mwa jiji la Bujumbura lakini walitimuliwa kwa mabomu ya moshi wa kutoa machozi.

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, amewaomba zaidi ya raia laki moja na hamsini waliokimbia ghasia nchini humo katika majuma kadhaa yaliyopita, warejee nyumbani. SOURCE: BBC SWAHILI
Posted by MROKI On Thursday, May 21, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo