Nafasi Ya Matangazo

March 11, 2015

Watu 42 wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa vibaya baada ya basi walilokuwa wakisafiria mali ya kampuni ya Majinja lenye bnamba za usajili T438 CED kuangukiwa na kontena baada ya kugongana na lori la mizigo Scania namba T 689 APJ, mali ya Cipex Company katika eneo la Changarawe, nje kidogo ya mji wa Mafinga mkoani Iringa leo.

Basi hilo lilikuwa likitokea mkoani Mbeya kwenda Dar es Salaam huku lori likitoka Dar es Salaam kwenda Mbeya.

Ubovu wa barabara katika eneo hilo inaelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ambacho kilichangiwa na mwendo kasi wa madereva na kutopeana mnafasi ya kupita eneo lenye mashimo. 

Vyombo vya uokoaji yakiwemo magreda yalifika katika eneo la tukio na kulitoa kontena hilo na shughuli za uopoaji wa maiti kufanyika kwa wananchi wakishirikiana na wanajeshi wa JKT Mafinga na askari wengine.
 
Basi hilo linadaiwa kuanza safari jijini Mbeya likiwa na abiria 37 lakini hadi wanafika eneo la ajali lilikuwa na abiria 64. 
Posted by MROKI On Wednesday, March 11, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo