Nafasi Ya Matangazo

March 28, 2015

SAM_1560
Diwani wa kata ya Ikoma wilaya ya Serengeti  mkoani Mara Sebastian Sabasaba Banagi akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari leo juu ya ujio wao kwa Mh.Lowassa, kuwa sauti ya wengi ni sauti ya Mungu hivyo kitendo cha kuzuiwa  wananchi kueleza hisia zao sio jambo la kidemokrasia bali linakandamiza uhuru wa kusema wanachokiamini huku akisisitiza kuwa Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli Edward Lowassa  ni chaguo la walio wengi na hawatasita kumtafuta popote kumueleza hisia zao(Habari Picha na http://jamiiblog.co.tz/
SAM_1575
Akizungumza na waandishi wa habari aliyekuwa katibu wa umoja wa wanawake wa {UWT} chama cha mapinduzi wilaya ya Serengeti Anna Mathayo Chacha alisema kuwa lowasa  ndie chaguo lao kwa kuwa ni kiongoziwanayeamini kuwa ataivusha nchi kutoka hapa ilipo ikiwa ni pamoja na kukipa heshima  na nguvu chama.
SAM_1564
Mkutano na wanahabari ukiwa unaendelea
SAM_1574
Diwani Viti maalum Bi.Kezia Magoko akitilia mkazo kuwa Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli Edward Lowassa ni chaguo la wengi
SAM_1571
Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi wilaya ya Serengeti Daniel Kegocha ambaye pia ni diwani aliomba chama hicho kuona umuhimu wa kumpitisha jina la Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli Edward Lowassa  kwa kuwa ni chaguo la walio wengi na yeyote anayetokea kupinga atakuwa ni msaliti katika chama hicho.
SAM_1573
Wadau wakifwatilia mkutano wao na wanahabari
SAM_1578Kushoto ni Magesa Nyamahiri,Emmanuel Nyawgaka,Julius Kirigiti wakiwa katika picha ya pamoja.
***********
WANANCHI wa wilaya ya Serengeti  mkoani Mara wamekitaka chama cha mapiduzi (CCM) kutokuzuia  demokrasia ya wanachama  kushawishi wagombea wa uraisi wanaona kuwa wanafaa kuwatetea kiti cha uraisi.
 
Wakizungumza   jana mkoani hapa,baada ya kufika nyumbani kwake  kwa  lengo la kumshawishi  Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli Edward Lowassa  kugombea nafasi ya uraisi ,wananchi hao walisema kuwa ni vyema chama kikawaacha wapenzi na mashabiki wa Lowassa kuendelea kumshawishi  agombee na nafasi hiyo.
 
Akizungumza na waandishi wa habari aliyekuwa katibu wa umoja wa wanawake wa {UWT} chama cha mapinduzi wilaya ya Serengeti Anna Mathayo Chacha alisema kuwa lowasa  ndie chaguo lao kwa kuwa ni kiongoziwanayeamini kuwa ataivusha nchi kutoka hapa ilipo ikiwa ni pamoja na kukipa heshima  na nguvu chama.
 
Aidha alisema kuwa wananchi wanahitaji utawala bora kwa sasa na mtu pekee ambaye wanadhani anatosha nafasi hiyo ni Edward Lowassa kwa kuwa ni kiongozi mwenye maamuzi magumu ambaye anaweza kusimamia utawala bora  hivyo viongozi wa ngazi za juu wasizue demeokrasia ya wananchi kusema ambacho wanahisi ni sahihi kwao.
 
Diwani wa kata ya Ikoma Sebastian Sabasaba Banagi alisema kuwa sauti ya wengi ni sauti ya Mungu hivyo kitendo cha kuzuiwa  kwa wananchi kueleza hisia zao sio jambo la kidemokrasia bali linakandamiza uhuru wa kusema wanachokiamini.
 
Alisema kuwa ili suluhu ya chama cha mapinduzi kushinda katika uchaguzi mkuu ni kumpitisha Lowassa kwa kuwa wao kama viongozin ambao wanawawakilisha wananchi na wananchi wanapendekeza kiongozi huyo kuwania kiti hcho kutokana na  matumaini na imani kubwa walioyo nayo kwake.
 
“kama alivyosema Waziri mkuu mstaafu ,Lowassa kuwa huwezi kuzuia mafuriko kwa mikono ni sahihi kabisa hata sisi tunaliunga mkono hilo hakuna mtu yeyote anayeweza kuzuia hisia za watu juu ya kiongozi huyu mahiri”alisema Banagi
 
Kwa upande wake mjumbe wa halmashauri kuu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Serengeti Daniel Kegocha aliomba chama hicho kuona umuhimu wa kumpitisha jina la mgombea huyo kwa kuwa ni chaguo la walio wengi na yeyote anayetokea kupinga atakuwa ni msaliti katika chama hicho.
 
Alisema kuwa, ni vizuri  kamati kuu ya chama kukaa chini kwa pamoja kutafakari na kuona umuhimu mkubwa wa kumpitisha mgombea huyo  kwa kuwa kila kona ya nchi wana imani naye na wana amani atawaletea maendeleo na kuliunganisha Taifa.
 
Wanachi hao kutoka wilayani Serengeti wakiongozwa na madiwani ,wananchi wa kawaida na waiowahi kushika nyadhifa katika chama hicho wapatao 65 wamefika wilayani Monduli ili kumshawishi mbunge huyo kutokata tamaa na kuendelea na nia ya kuchukua fomu huku wakiahidi kuwa ni watamfuata alipo ili kumshawishi na kuzungumza nae.
Posted by MROKI On Saturday, March 28, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo