Nafasi Ya Matangazo

January 25, 2015

Timu za soka za Simba na Azam leo zimetoka sare ya bao 1-1 katika mchezo wa ligu kluu soka Tanzania uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Mabao hayo yalifungwa na Emmanuel Okwi upande wa Simba na Kipre Cheche upande wa  Azam.

Aidha katika mchezo huo Mshambuliaji mganda wa Simba, Emmanuel Okwi aligongana na Agrey Moris na klupoteza fahamu jambo ambalo lilipelekea kutolewa nje ya uwanja kwa machela na vbaade kupelekwa Muhimbili kwa matibabu zaidi

Pichani ni Okwi akiwa chini uwanjani huku daktrai wa Simba Yassin Gembe akitoa huduma ya kwanza kabla ya mwamuzi kuomba atolewe nje kwa matibabu zaidi. 

Aidha kwa mujibu wa daktari huyo wa Simba, Yassin Gembe, Okwi aligongwa sehemu ya kichwa na kupelekea kupoteza fahamu na yupo Muhimbili kwa matibabu zaidi na hali yake inaendelea vizuri na kuwatoa hofu mashabiki na wapenzi wa Simba.
Posted by MROKI On Sunday, January 25, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo