Nafasi Ya Matangazo

December 18, 2014

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Makazi,Profesa Anna Tibaijuka amesema kuwa hawezi kujiuzulu katika nafasi  ya uwaziri kutokana fedha ya Tegeta ESCROW. 
 
Akizungumza  na Waandishi na Habari mapema leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Hoteli ya Hayyat Regency, Profesa Tibaijuka  alisema kuwa udalali wake wa  fedha hiyo ni kwa ajili ya wanafunzi katika shule  za Taasisi ya  Barbo Johansson  Girls Education Trust, na kwamba fedha aliyoipata ni  Bilioni  Tshs. 1.66 ambazo zilitoka katika kampuni ya James Rugemalira kama msaada kwa shule hiyo.
 
Alisema kuwa fedha hiyo kuingia katika akauti yake binafsi ilitokana na masharti ya mtoa msaada ndugu James  Rugemalira  ambaye alitaka fedha hiyo iingie katika akauti ya Benki ya Mkombozi. 

"Nikijiuzulu hata Rais Jakaya Kikwete atanishangaa kwani fedha nilizopata ni za shule na kwa ajili kukomboa elimu nchini  hasa kwa watoto wa kike kutokana na wazazi wengi kutoweza kumudu gharama za shule’’alisema.

Alisema kuwa udalali wake ni kutafuta  fedha kwa ajili ya elimu nchini ambapo, alidai hata Mwenyekiti wa Makampuni  ya IPP  Dkt Reginald Mengi alitoa sh.milioni 248 kwa ajili ya msaada wa shule hiyo.

Profesa Tibaijuka  alisema kuwa  wananchi watambue kuwa yeye ni mstaafu wa Umoja wa Mataifa hivyo hawezi kufanya hivyo na kama angetaka fedha hiyo angeweza kufuata hata katika shule na kuchukua.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi,Profesa Anna Tibaijuka akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es salaam leo.
 Sehemu ya Waandishi wa Habari waliofika kwenye Mkutano huo ulioitishwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi,Profesa Anna Tibaijuka. 
NA CHALILA KIBUDA WA MICHUZI MEDIA.
Posted by MROKI On Thursday, December 18, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo