Nafasi Ya Matangazo

November 24, 2014

Na MatukiodaimaBlog
MBUNGE  wa   viti maalum  mkoa  wa  Iringa Ritta Kabati (CCM) amewakata   wananchi  kutokubali kudanganywa na  vyama  vya  siasa  vinavyounda umoja wa katiba  ya  wananchi (UKAWA)  juu ya mchakato  wa  katiba  iliyopenekeshwa  na badala yake  kuungana na  watanzania wapenda maendeleo  kuikubali  katiba   hiyo  muda  utakapofika.

Mbuge Kabati  alitoa  kauli   hiyo kwa nayakati  tofauti juzi na  jana  wakati  wa  semina  zake za  ndani na wanawake  wanachama  wa UWT  katika wilaya ya  Iringa , Kilolo na Mufindi semina  iliyolega  kuwajengea  uwezo  wa  kujiamini kwa  wanawake  waliojitokeza  kugombea nafasi  mbali  mbali  za  uongozi wa  serikali  za mitaa na  vijijini .

" Mimi  kama  mbunge  wa  viti maalum  mkoa  wa Iringa   wajibu   wangu  ni pamoja na kukutana na  wananchi  wa  Iringa na  kuwajengea  uelewa   mpana  wa  katiba  hiyo  iliyopendekezwa  ila  muda  ukifika  wa  serikali  kutangaza mchahato  wa  kupokea maoni ya  wananchi   juu ya katiba   hiyo  iliyopendekezwa  basi   viongozi hao  waweze  kuelewa  zaidi  pamoja na  wananchi  wanaowazunguka..... hivyo  nitaendelea  kutoa  elimu  kwa  viongozi  wa chama katika  semina  mbali mbali"

Kabati  alisema   kumekuwepo na  upotoshwaji  mkubwa ambao  umeendelea   kufanywa na UKAWA  kwa  kuzunguka  huku na kule  kujaribu  kupotosha  ukweli    juu ya katiba   iliyopendekezwa  kwa madai  kuwa  ni katiba ya  CCM jambo ambalo  ni upotoshaji mkubwa na  kuwa  mchakato  wa katiba    hiyo  ulifanywa na vyama vyote  na makundi  maalum.

Pia  alisema  kuwa  kitendo  cha  baadhi  ya  wanasiasa  wasilolitakia  mema  Taifa hili kwa  kupotosha   juu ya katiba   hiyo ni  sawa na  kutaka  kuona  nchi haitawaliki   na   hivyo  kuamua  kuanza  upotoshaji  huo.


 Alisema  kuwa  si  kweli kama katiba  hiyo  iliyopendekezwa  haina jambo  lolote la msingi kama  ambavyo  UKAWA  wamekuwa  wakizunguka na  kupotosha  ila alidai kuwa ndani ya katiba   hiyo  kuna mambo  mengi  yamezingatiwa  kwa  ajili  ya  wananchi  na  Taifa   kwa   ujumla.


Akielezea  kuhusu  mchakato  wa uchaguzi  wa  serikali  za  mitaa ,vijiji na vitongoji  unaotaraji  kufanyika  hivi karibuni  alisema  kuwa  upande  wa  mkoa  wa  Iringa  wanawake  baada ya  kuhamasishwa  wamepatika  kujitokeza  kwa   wingi  kuchukua  fomu  za  kuwania nafasi mbali mbali  za  uongozi na kuwa  baadhi ya maeneo  wamepata  kushinda kwa  kishindo nafasi  walivyoomba ndani ya CCM wakisubiri  uchaguzi  rasmi wa serikali .

Hivyo aliwataka  wananchi wa  mkoa  wa Iringa  kujitokeza  kuwapa kura  zao  wanawake hao  waliogombea nafasi mbali mbali na  kuwa  imani  yake  kuona kunakuwa na uongozi mchanganyiko.
Posted by MROKI On Monday, November 24, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo