Nafasi Ya Matangazo

November 25, 2014

Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya BAF (Brigitte Alfred Foundation) na Miss Tanzania 2012,Bi. Brigitte Alfred akimtumza mmoja wa vijana wenye ulemavu wa ngozi (albino) ambao wako chini ya Taasisi hiyo,aliekuwa akighani shairi alilolitunga,wakati wa hafla ya kusherehekea Mafanikio ya Vijana hao iliyofanyika leo kwenye Viwanja Makumbusho,Jijini Dar es Salaam.Taasisi ya BAF kupitia Mpango wake wa JA (Juniour Achievement) imeweza kuelimisha vijana 50 wenye ulemavu wa ngozi katika mpango wa kutoa elimu ya kujitambua, ujasiriamali na stadi za biashara ili waweze kuthubutu, kuanzisha na kuendeleza biashara na shughuli nyingine za kiuchumi zitakazo wapa ajira, kipato na kuinua ustawi wa maisha yao na familia zao.

Kijana mwenye ulemavu wa ngozi (albino) akighani mashairi yake.
Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya BAF (Brigitte Alfred Foundation) na Miss Tanzania 2012, Bi. Brigitte Alfred akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Pugu waliofika kwenye hafla hiyo ya kusherehekea Mafanikio ya Vijana,yaliyofanyika leo kwenye Viwanja Makumbusho,Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya BAF (Brigitte Alfred Foundation),Bi. Brigitte Alfred akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya vijana wenye ulemavu wa ngozi (albino) ambao wako chini ya Taasisi hiyo.
Baadhi ya Wanahabari waliohudhulia hafla hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya BAF (Brigitte Alfred Foundation) na Miss Tanzania 2012,Bi. Brigitte Alfred pamoja na baadhi ya vijana wenye ulemavu wa ngozi (albino) ambao wako chini ya Taasisi hiyo. SOURCE: MICHUZI MEDIA.
Posted by MROKI On Tuesday, November 25, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo