Nafasi Ya Matangazo

November 24, 2014

Meneja Masoko na Mauzo wa Azma Media, Mgope Kiwanga (kushoto),Ofisa Masoko na Mauzo, Shah Mrisho (kati) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited, Rhys Torringotn wakiwa katika mkutano na wanahabari Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa Promosheni ya 'Mtonyo Chapchap' ya Azam TV, iliyoanza leo na itaendelea hadi Desemba 31, mwaka huu. 
Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited, Rhys Torringotn (kulia) akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam makao makuu ya kampuni hiyo, TAZARA,kuhusu promosheni ya hiyo ya 'Mtonyo Chapchap' ya Azam TV, ambayo imeanza leo na itaendelea hadi Desemba 31, mwaka huu. Pamoja nae ni Meneja Masoko na Mauzo, Mgope Kiwanga.
Azam Media Limited leo wamezindua rasmi promosheni ya 'Mtonyo chapchap' ambayo ni moja ya shamra shamra zake za kutimiza mwaka tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo. 
Mtonyo Chapchap itadumu hadi Desemba 31 mwaka huu  na itampatia mteja gharama ya fedha aliyotumia kununua kisumbusi ambayo ni shilingi 165,00/= .
Mteja anaetaka kuingia katika droo hiyo, anatakiwa kununua kisumbusi kipya vya Azam TV na kukiwekea malipo ya mwezi na promosheni hiyo itawahusu wateja wapya na wazamani.
Kutakuwa na  washindi 100 watakaopatikana katika kipindi chote cha kampeni hiyo ambao watakuwa wakitangazwa kila wiki kupitia kwenye vyombo habari, mbalimbali kama vituo vya Radio, Televisheni, Magazeti na magazeti tando (blogu). 
Wiki ya kwanza, watangazwa washindi 15, kama ambavyo itakuwa katika wiki ya pili, wakati ya tatu watatangazwa washindi  20 kabla ya wiki ya mwisho kutangazwa washindi 50.
Posted by MROKI On Monday, November 24, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo