Nafasi Ya Matangazo

October 23, 2014


Mshindi wa taji la Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu huenda akavuliwa taji hilo kama serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Baraza lake la Sanaa la Taifa ambalo ndio watoaji vibali vya mashindanio hayo na kusimamia dhima na maudhui ya shindano hilo pamoja na kusimamia maadili yake itaingilia kati moja kwa moja suala hilo kwa kuunda tume maalum ya kulichunguza na kutafuta ukweli halisi wa umri wa mrembo huyo na kutoa mapendekezo ya ama Sitti avuliwe taji hilo na kuvikwa Mshindi wa pili, Lillian Kamazima (pichani kulia) ama vinginevyo.

Kushoto ni Jihhan Dimachk aliyeshika nafasi ya tatu.

Shindano la Miss Tanzania 2014 lilifanyika katika ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam Oktoba 11,  na Sitti Mtemvu kuvikwa taji hilo na kuanza utata wa umri wake halisi licha ya kuanika hadharani cheti chake cha kuzaliwa ambacho wadau wa sanaa ya urembo kukitilia shaka na kushindwa kuoanisha na pasi yake ya kusafiria na leseni ya udereva iliyotolewa nchini Marekani. 
Posted by MROKI On Thursday, October 23, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo