Nafasi Ya Matangazo

September 12, 2014



MOJA ya sifa ya mwandishi ni kusoma, na katika kusoma huko na kupekua pekua hapa na pale unaweza kujifunza na kupata la kuandika kupitia maandiko ya watu wengine na kutoa elimu kwa umma. Leo nimepita pita katika kurasa za marafiki zangu huko katika uso wa kitabu ‘Facebook nikakutana na nasaha ya ndugu yangu Victory Richard, juu ya kuwasihi wanawake kwamba  sasa wavae nguo.

Ndugu yangu yule amechoshwa na tabia za dada zetu, wake zetu na hata mama zetu wakati mwingine wanavyotembea uchi, ndio! utavaaje nguo fupiii au skintight halafu useme umevaa nguo?. Binafsi naomba radhi kama nitakuwa nimemkwaza mtu hasa hao mama zetu, Ah! Lakini potelea mbali Anko Kidevu sijali kitu si wamejitakia.

Hivi akina mama na dada zetu kweli jamani katika yooote ambayo mnalilia usawa na sisi tunakubali kuwa sawa, hili la kutembea uchi au kuvaa mavazi nusu uchi mbona mnapitiliza?

Ndio mmepitiliza Anko nimebaini kuwa mmetupita maana sisi tukivaa sana ni kaptura au bichkoma na kawosh au singlendi lakini sasa naona mmepita katika sketi na sasa mna vimini na kuacha vifua wazi.

Ni nani awezaye kuona aibu yenu zaidi yangu mimi Anko Kidevu na kaka yenu Victor Richard, tafadhalini tunawasihi, hebu vaeni nguo sasa na jamii itawaheshimu maana hakuna heshima kwa mwanamke hata kidogo. Na kama mnahisi mnaheshimika kwa hilo ni bure kabisa.

Hivi sasa thamani ya mwanamke haipo tena hapa nchini kwetu hasa mijini, sijui huko kwa wenzetu maana hapa nchini hivi sasa ili mwanamke aonekane katika jamii lazima avue nguo, akitaka aonekane mshereheshaji mzuri lazima avue nguo, ili uonekane wewe ni mwigizaji bora au mwimbaji bora lazima uvue nguo, na ili uonekane mzuri lazima uvue nguo.

Nini hasa mnakitafuta jamani ninyi wana wa adama? Unajua mimi nilianza kuona zamani thamani yenu inashuka tangu nilipoanza kuona nguo zenu za ndani zikiuzwa hadharani madukani.

Kweli kabisa hazadharani!! Mlipoona ya madukani haitoshi mkaamua sasa mkizivaa zionekane pia na kujichoresha maungo yenu. Wengine mikorogo imewaharibu imebaki michirizi kama shamba lililovunwa mpunga kule Kinyenze.

Unajua zamani kukuta muuza duka ametundika nguo ya ndani ya kike anaiuza ili kuwa nadra! Lakini zile VIP zetu zilikuwa hadharani unaziona hata ukienda duka la pipi, lakini sasa naona mambo yamaebadilika, nguo za kiume huzioni zikiwekwa wazi madukani bali hizo zenu kwanza ndio kivutio mlangoni, acheni bwana tumechoka inatosha.

Hivi na nyie serikali mpo wapi sasa maadili mnaanzia kuyalinda wapi? Au katika m,ashindamno ya umiss tu lakini huku mtaani hakuna? Sijui ni wizara gani mnahusika au ni idara ya Utamaduni? Mnaonaje na nyie mkianza kamata kamata kama ya boda boda ukiingia mjini na kimini au skini taiti ndani ya karandinga hao mahakama ya sokoine fine au jela.

Kwanza jiji kwa taarifa yenu nshawapa dili la kukuza mapato yenu au idara yaUtamaduni pale kwa mama yangu Dk. Fenela Mukangara mtakuwa mmejiongezea kipato.

Unajua hivi sasa magazeti, kurasa za mitandao yua kijamii inayosomwa sana ni ile iliyo na picha zenu za uchi? Hili ndo limepawa ukilema baadhi ya waandaji wa majarida na filamu ili bidhaa zao zionekane bora na zipate soko lazima mwanamke avuliwe nguo.

Wamama zetu ndio waandaaji wakubwa wa shughuli za kuwatoa wali au watoto ndani ni nyie ajabu mnaalika vikundi vya wamama wenzenu wa kucheza uchi ili shughuli inoge.

Umama na udada wenu umegeuzwa kuwa bidhaa. Wenye kupaza sauti wamekaa kimya si kwamba hawalioni hili la hasha....wengi wao ni wanawake wanaogopana, yuko wapi mama yangu Hellen Kijo Bisimba na dada yangu Ananilea Nkya wanaharakati wa haki za binadamu je hamuoni haja ya kuanzisha harakati za kupinga wanawake wanao vaa nguo za kulalia barabarani?. Ama mwaogopa mkipaza sauti juu ya hili mkaa uchi atamuhukumu siku ikifika.Sijui naawachia ninyi.

Napongeza wizara ya mambo ya Ndani ya Nchi pale msichana amevaa uchi haingii, kanguo kako ka kubana huko huko. Hebu nanyie katika ofisi zenu igeni basi.
Posted by MROKI On Friday, September 12, 2014 1 comment

1 comment:

  1. kwanza kabisa, duniani mwote hakuna mtu/mwanadamu awezaye kutembea uchi bila ya kukaliwa na roho chafu/mapepo - kumbuka adamu na hawa walivyojigundua wa uchi.
    wapo wanawake wa aina mbili
    1. wanaojilazimisha kutovaa nguo mpaka mapepo maimuna yanawaingia na kufanya tabia ndani mwao
    2. wale ambao kwa asili kutokana na mapokeo wana roho tu chafu na hivyo hiyo ni tabia

    marekebisho ya kiroho yanatakiwa kwa wanawake ili washinde hali hizi

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo