Nafasi Ya Matangazo

July 25, 2014

WAKATI bado kukiwa na sinto fahamu juu ya hatma ya Chuo cha Sayansi ya Tiba cha IMTU ambacho kinakabiliwa na tuhuma ya kuhusika na utupaji wa viungo vya Binadamu vilivyokuwa vikitumika katika mafunzo chuoni hapo hivi karibuni Hospitali yake ya IMTU imefungiwa.

Hospitali ya IMTU iliyopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam imefungiwa kufanya kazi zake kutokana na makosa mbali mbali ya kiutalaam lakini kubwa ni kukosa wafanyakazi wa kutosha na kutoa huduma bila ya kuwa na vifaa stahiki huku wakitumia madawa ambayo yamepitwa na muda wake.

Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya kufanyika kwa ukaguzi Hospitalini hapo na vyanzo vinapasha hilo halina uhusiano na upande wa Chuo cha IMTU ambao unatuhumiwa kutupa viungo vya binadamu vuilivyokuwa vikitumiwa katika mafunzo chuoni hapo.
Posted by MROKI On Friday, July 25, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo